Mr. Christopher Simwimba
Mr. Christopher M. Simwimba
The Head of Department
(DAICO)

Utangulizi

Idara ya Kilimo Umwagiliaji na Ushirika ni moja kati ya Idara zinazounda Halmashauri ya wilaya ya Meatu. Kazi kubwa ya Idara hii ni kutoa huduma za ugani kwa wakulima kwa lengo la kuboresha tija na kiwango cha uzalishaji wa mazao ya kilimo. Idara hii pia inajihusisha na usimamizi na uendelezaji wa shughuli za Ushirika kupitia vyama vya ushirika vya msingi vya mazao ya kilimo (AMCOS) na SACCOS.

Idara hii imegawayika katika vitengo 2 ambavyo ni; Kitengo cha Kilimo na Kitengo cha Ushirika. Hivi sasa idara inayo watumishi 58 wa fani mbalimbali kuanzia ngazi ya vijiji, kata, tarafa na wilaya.

Hali ya Kilimo

Kwa zaidi ya asilimia 90 ya uchumi wa Wilaya hutegemea kilimo cha mazao mbalimbali. Mazao makuu ya chakula yanayolimwa ni Mtama, Mahindi, Viazi vitamu, Mpunga na Mikunde. Mazao makuu ya biashara ni Pamba, Alizeti, Ufuta na Choroko.