Teknolojia ya Habari, Mawasiliano na Uhusiano (TEHAMA)
Kitengo cha (TEHAMA) katika Halmashauri ya Wilaya ya Meatu ambacho ni muunganiko wa Kitengo cha IT na Uhusiano kinaongozwa na Sera ya TEHAMA (2003), na Sera ya Utangazaji Habari (2004) pamoja na mwongozo wa wakala wa serikali mtandao(eGA).
Ibara ya 18 yakatiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaeleza kuwa
1) Bila ya kuathiri sheria ya nchi, na kutafuta,kupata na kueneza au kusambaza habari na mawazokupitia chombo cha habari chochote bila ya kujali mipaka ya taifa pia anayohakina uhuru wa kutoingiliwa na mawasiliano
2) Kila raia ana haki ya kupashwahabari wakati wote kuhusu matukio mbalimbali ya nchini na duniani kote yenyeumuhimu kwa maisha na shughuli za wananchi , pia kwa masuala yenye umuhimu kwajamii.
Majukumu ya Kitengo
HUDUMA
|
HUDUMA ZITOLEWAZO
|
JINSI ZINAVYOPATIKANA
|
1
|
Kutoa habari kwa Wananchi, taarifa za robo au mwaka kwa wananchi na wadau wa maendeleo kuhusu masuala yanayogusa jamii.
|
- Tovuti ya Halmashauri (www.meatudc.go.tz)
- Vipeperushi - Barua pepe - Magazeti, n.k. |
2
|
Kusimamia ufikishwaji wa huduma za mawasiliano kwa wananchi
|
- kampuni za mawasiliano ya simu
|
3
|
Kusaidia jamii kuwa na weledi wa masuala ya mitandao na kuweza kujilinda dhidi ya mashambulizi.
|
- Tovuti ya Halmashauri
- Vipeperushi - Semina na warsha. |
4
|
Kutathimini na kusimamia viashiria vya hatari kuhusiana na miundombinu na mifumo ya TEHAMA
|
- Kuwasiliana na wataalam wa TEHAMA waliopo Halmashauri.
|
5
|
Miongozo kuhusu mabadiliko ya njia za utoaji huduma mbalimbali za kielektroniki.
|
- Tovuti ya Halmashauri
- Matangazo - Vipeperushi na semina. |
6
|
Kusimamia mifumo ya kielektroniki ya usimamizi wa fedha, takwimu na ukusanyaji mapato ya ndani, takwimu, n.k.
|
- Benki
- Mitandao ya Epicor, LGRCiS, BEMIS, HCMIS, FFARS, SIS - Mtandao wa intaneti |
7
|
Kufanya usimikaji na uhuishaji wa programu za kompyuta, na matengenezo ya vifaa vya TEHAMA.
|
- Kufika Kitengo cha TEHAMA
- Kuwasiliana na wataalam wa TEHAMA kwa simu au barua pepe. |
8
|
Kutoa ushauri kuhusu matumizi ya vifaa vya TEHAMA.
|
- Kufika Kitengo cha TEHAMA
- Kuwasiliana na wataalam wa TEHAMA |
9 | Kusimamia mifumo ya hifadhi ya Jamii - CHF iliyoboreshwa kuhakikisha kaya zinasajiliwa kwenye mfumo | Kuwasiliana na maafisa waandikishaji ngazi ya vijiji, wafawidhi, waratibu au kufika Ofisi ya Kitengo cha TEHAMA
|
CHANGAMOTO ZA KITENGO
Licha ya Kitego kuwa na changamoto zilizotajwa hapo juu, Kitengo kimefanikiwa kuwa na watumishi wawili
Kitengo Kinaongozwa na
1. Ndg. Vicent Mapalala (Afisa TEHAMA)
Simu 0762 326 992
Barua pepel: vicent.mapala@meatudc.go.tz
2. Ndg. Linus R. James(Afisa TEHAMA)
Simul: 0686 654 499
Barua pepel: linus.james@meatudc.go.tz
Meatu, Simiyu, Tanzania
Anwani ya Posta: S.L.P 44
Simu: 028 2795 008
Simu ya Mkononi: 0622 404 712
Barua Pepe: ded@meatudc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meatu . Haki Zote Zimehifadhiwa.